• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango takwimu na Usuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uru kaskazini
    • Kata
      • Arusha chini
      • Kahe
      • Kahe mashariki
      • Kibosho kati
      • Kibosho kati
      • Kibosho magharibi
      • Kibosho mashariki
      • Kilema kaskazini
      • Kilema kati
      • Kilema kusini
      • Kimochi
      • Kindi
      • Kirima
      • Kirua vunjo kusini
      • Kirua vunjo magharibi
      • Kirua vunjo mashariki
      • Mbokomu
      • Mabogini
      • Makuyuni
      • Mamba kaskazini
      • Mamba kusini
      • Marangu magharibi
      • Marangu mashariki
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kusini
      • Njia panda
      • Okaoni
      • Old moshi magharibi
      • Old moshi mashariki
      • Uru kaskazini
      • Uru kusini
      • Uru mashariki
      • Uru shimbwe
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogondogo
  • Kituo cha Habari
    • Gallery

PROF TUMAINI NAGU AKAGUA HUDUMA ZA AFYA MOSHI DC, ASISITIZA UBORA NA UWAJIBIKAJI

Posted on: February 23rd, 2026

PROF TUMAINI NAGU AKAGUA HUDUMA ZA AFYA MOSHI DC, ASISITIZA UBORA NA UWAJIBIKAJI


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayesimamia masuala ya Afya, Prof. Tumaini Nagu, amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kukagua mifumo ya utoaji huduma, utendaji kazi wa watumishi, pamoja na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya.


Katika ziara hiyo, Prof. Nagu aliambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na wataalamu wa ngazi ya mkoa na wilaya.


Prof. Nagu na timu yake alitembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi iliyopo Kata ya Mabogini, ambapo alikagua wodi mbalimbali, maabara, duka la dawa na mifumo ya TEHAMA inayosimamia mfumo wa GOTHOMIS katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na kutunza taarifa za wagonjwa. Pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa afya na kusisitiza umuhimu wa uwajibikaji, weledi na utoaji wa huduma kwa kuzingatia maadili ya taaluma.


Aidha, alitembelea Kituo cha Afya cha Uru Kusini ambako alikagua miundombinu ya jengo la mama na mtoto, chumba cha dharura pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. Alielekeza uongozi wa halmashauri kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.


Akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya na Kituo cha afya cha Uru Kusini, Prof. Nagu alisisitiza uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa kuzingatia maadili ya taaluma.


“Serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Ni wajibu wenu kuhakikisha uwekezaji huu unaleta matokeo chanya kwa kutoa huduma bora, zenye utu na kwa wakati,” alisema Prof. Nagu.


Aliongeza kuwa usimamizi madhubuti wa rasilimali watu na vifaa tiba ni msingi wa kuimarisha imani ya wananchi kwa huduma za afya za umma.


Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Jair Khanga alisema mkoa utaendelea kushirikiana na halmashauri kuhakikisha viwango vya utoaji huduma vinaimarika na matumizi ya mifumo katika kutoa huduma inasimamiwa vizuri.


“Tutaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha changamoto zinazobainika zinapatiwa ufumbuzi wa haraka na huduma zinatolewa kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa,” alisema Dkt. Khanga


Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Dkt Juma Mombokaleo alieleza kuwa ziara hiyo imekuwa chachu ya kuongeza morali kwa watumishi na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho zaidi na kuomba muda wa mwezi mmoja kurekebisha kasoro ndogondogo zilizobainishwa.


“Maelekezo tuliyoyapata yatatusaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa huduma, hususan katika maeneo ya dharura, afya ya mama na mtoto na upatikanaji wa dawa pamoja na matumizi ya mfumo wa GOTHOMIS” alisema Dkt Mombokaleo.


Ziara hiyo imelenga kuimarisha usimamizi, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya na kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinatumika kama ilivyokusudiwa kwa manufaa ya wananchi.




Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU December 31, 2025
  • KATAZO LA KUPAKIA, KUSHUSHA ABIRIA NA MIZIGO NJE YA VITUO VYA MABASI MAMLAKA YA MJI MDOGO WA HIMO. January 02, 2026
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI 29-01-2024 January 29, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III NA NAFASI YA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II TAREHE 06.02.2024 February 06, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • PROF TUMAINI NAGU AKAGUA HUDUMA ZA AFYA MOSHI DC, ASISITIZA UBORA NA UWAJIBIKAJI

    February 23, 2026
  • WAZIRI MKUU DKT MWIGULU NCHEMBA ARIDHISHWA NA UBORA WA JENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

    February 20, 2026
  • RC BABU AFUNGUA MAFUNZO YA MADIWANI MOSHI DC, WAASWA KUZINGATIA KANUNI, SHERIA NA TARATIBU.

    January 20, 2026
  • DC MNZAVA ASISITIZA WAZAZI KUPELEKA WATOTO SHULE

    January 15, 2026
  • Tazama yote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • report za halmashauri

Viunganishi linganifu

  • Tovuti Kuu ya serekali
  • Tovutu ya serekali mtandao (eGA)
  • Tovuti ya Mkoa Kilimanjaro
  • Tovuti ya wizara ya tamisemi
  • Tovuti ya wizara ya fedha
  • Tovuti ya wizara ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Muelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji

    Sanduku la posta: P.o.Box 3003 Moshi

    Simu ya Mezani: Phone 2751865

    Mobile:

    Barua pepe: Email : ded@moshidc.go.tz or info@moshidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma
    • Sera ya faragha

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Haki zote Zimeifadhiwa.